Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 20:57

Watu wawili washikiliwa nchini Denmark


Watu wakiweka mashada ya mauka katika hrkslu ls esyshufi mnjini Copenhagen, Denmark, Jumatatu, Ferbuari, 16, 2015.
Watu wakiweka mashada ya mauka katika hrkslu ls esyshufi mnjini Copenhagen, Denmark, Jumatatu, Ferbuari, 16, 2015.

Polisi wa Denmark, inawashikilia watu wawili wanaodaiwa kumsaidia mshambuliaji aliyeua watu wawili katika matukio tofauti mjini Copenhagen, siku ya jumamosi.

Polisi Jumatatu wamesema kwamba watu hao wawili ni washukiwa waliomsaidia mshambuliaji wa matukio hayo.

Mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 22 alishambulia kwa kufyatua risasi mjadala juu ya uhuru wa kujieleza na katika hekalu la wayahudi, mjini Copenhagen.

Waziri mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schidt, ameyaita mashambulizi hayo mawili kama kitendo cha chuki cha kigaidi dhidi ya Denmark.

Polisi walimua mshambuliaji huyo mzaliwa wa Denmark, siku ya Jumapili baada ya kuwashambulia maafisa wa polisi.

XS
SM
MD
LG