Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 06:57

Watu zaidi ya milioni 1.5 waomba kibali maalum kuingia Qatar


Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hamad Doha Qatar. (REUTERS)
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hamad Doha Qatar. (REUTERS)

Qatar ilisema Jumapili kwamba zaidi ya watu milioni 1.5 wameomba pasi ya ya kuingia kwenye  Kombe la Dunia la kandanda, linaloanza Novemba 20.

Saad Al-Suwaidi, mkuu wa huduma ya pasi ya Hayya, alisema kati ya watu milioni 1.5 na milioni 1.7 hadi sasa wametuma maombi ya kadi hiyo, ambayo inafanya kazi kama visa, tiketi ya mechi, tiketi ya usafiri na inatoa fursa ya kuingia katika baadhi ya maeneo ya mashabiki.

Wasafiri wote kwenda Qatar watahitaji pasi ili kuingia kuanzia Novemba 1, wawe wanakusudia kutazama mchezo au la.

Qatar imesema inatarajia wageni zaidi ya wageni milioni 1 pamoja na maelfu ya mashabiki wa ndani.

Washabiki wa kimataifa lazima waombe pasi baada ya kununua tiketi na kupata malazi.

​Viwanja vya ndege viwili vya kimataifa vya Doha vinajiandaa kushughulikia wageni 150,000 kwa siku, maafisa walisema.

Wale wanaovuka kwa magaei kutoka Saudi Arabia lazima wapande basi hadi Doha au walipe ada ya $1,375 ili kuendesha magari yao wenyewe.

XS
SM
MD
LG