Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 22:33

Watu zaidi washuhudiwa wakielekea Uingereza baada ya wahamiaji 12 kufariki


Miili ya wahamiaji waliofariki baada ya kujaribu kuvuka kivuko cha Uingereza huko Boulogne-sur-Mer, kaskazini ,mwa Ufaransa, Septemba 3, 2024.
Miili ya wahamiaji waliofariki baada ya kujaribu kuvuka kivuko cha Uingereza huko Boulogne-sur-Mer, kaskazini ,mwa Ufaransa, Septemba 3, 2024.

Siku chache baada ya wahamiaji 12 kufariki walipokuwa wanajaribu kuvuka kivuko cha Uingereza kutoka kaskazini mwa Ufaransa, boti nyingine iliyokuwa imebeba darzeni ya watu imeonekana ikijaribu kufanya safari kama hiyo leo Jumatano, ikielekea Uingereza.

Kulingana na waandishi wa shirika la habari la Associated Press waliokuwa kwenye ufukwe wa bahari wa Wimereux, kwenye pwani ya kaskazini mwa Ufaransa, na karibu na mahali ajali ya jana Jumanne ilitokea, boti ya kutumia hewa imeonekana ikiwa imebeba watu, wanaodhaniwa kuwa wahamiaji.

Boti hilo imeonekana kujaa watu wengine miguu ikiwa nje ya boti.

Wengi wao walikuwa wamevalia fulana za kuokoa maisha wakati wa ajali.

Boti ya doria, yenye bendera ya Ufaransa imekaribia boti hiyo lynye wahamiaji na kuonekana kuwapa fulana za rangi ya manjano za kuokoa maisha.

Idadi kubwa ya waliofariki jana jumanne, walikuwa wanawake na wasichana wadogo. Wengi wao hawakuwa wamevaa fulana za kuokoa maisha na ajali hiyo imetajwa kuwa mojawapo ya ajali mbaya zaidi za boti kwenye kivuko hicho.

Forum

XS
SM
MD
LG