Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:35

Watu watatu wauawa katika shambulio dhidi ya makanisa mawili Nigeria


Majeneza yapangwa wakati wa ibada ya maombolezi kwa waathirika waliouawa katika shambulio la watu wenye silaha wakati wa ibada ya misa kwenye kanisa la mtakatifu Francis huko Owo, Ondo, Nigeria, June 17, 2022. Picha ya Reuters
Majeneza yapangwa wakati wa ibada ya maombolezi kwa waathirika waliouawa katika shambulio la watu wenye silaha wakati wa ibada ya misa kwenye kanisa la mtakatifu Francis huko Owo, Ondo, Nigeria, June 17, 2022. Picha ya Reuters

Watu wenye silaha Jumapili wameshambulia makanisa mawili katika eneo la vijijini kaskazini magharibi mwa Nigeria na kuua watu 3, mashahidi na afisa wa jimbo wamesema, wiki kadhaa baada ya shambulio kama hilo katika taifa hilo la Afrika magharibi kuua waumini 40.

Shambulio hilo katika eneo la Kajuru katika jimbo la Kaduna lililenga vijiji vinne, na kusababisha utekaji nyara wa wakazi ambao idadi yao haikuthibitishwa na uharibifu wa nyumba kabla ya washambuliaji kutoroka, wenyeji wamesema.

Haikufamika mara moja waliofanya shambulio hilo kwenye makanisa huko Kaduna.

Sehemu kubwa ya Nigeria imekuwa ikikumbwa na matatizo ya usalama, Kaduna ikiwa ni moja ya majimbo yaliyoathirika sana. Wiki iliyopita, watu 32 waliuawa katika eneo la Kajuru katika shambulio lililodumu saa kadhaa.

Waumini walikuwa wamehudhuria Jumapili asubuhi ibada ya misa kwenye kanisa la Kibaptist la Maranatha na kanisa la Katoliki la mtakatifu Moussa katika jamii ya Rubu ya Kaduna, wakati washambuliaji walifika eneo hilo na kuzingira makanisa hayo yote yakiwa katika eneo hilo, amesema Usman Danladi ambaye anaishi karibu na eneo hilo.

Serikali ya jimbo la Kaduna imethibitisha vifo vya watu 3 waliouawa na majambazi ambao walivamia vijiji wakiwa kwenye pikipiki.

Shirika la kikatoliki la Nigeria limelaani mashambulizi ya Jumapili na kusema kwamba makanisa nchini Nigeria yamekuwa yakilengwa na makundi yenye silaha.

XS
SM
MD
LG