Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:17

Watu wapatao 18 wamefariki nchini Sudan Kusini


Ghasia za kisiasa huko Sudan Kusini zapelekea watu kukosa makazi
Ghasia za kisiasa huko Sudan Kusini zapelekea watu kukosa makazi

Watu wasiopungua 18 waliuwawa katika mgogoro wa silaha uliozuka Alhamis usiku kwenye eneo la Protection of Civilians katika mji wa Malakar nchini Sudan Kusini.

Vifo hivyo vimewahusisha wafanyakazi wawili wa kundi la Madaktari wasio na mipaka-MSF waliopo Sudan Kusini ambao walishambuliwa katika nyumba zao, taasisi hiyo ilisema.

Timu zilifanya kazi usiku kucha kuwahudumia majeruhi 36 kwenye hospitali ya MSF mjini Malakar ilisema wagonjwa wasiopungua 25 walikuwa na majeraha ya risasi na wanane walihitajika kufanyiwa upasuaji. Maiti zaidi zinaendelea kuwasili hospitalini hapo.

Ghasia hizi awali ziliwalazimisha kiasi cha watu 600 wengi wanawake na watoto kukusanyika ndani ya hospitali.

Familia zinaishi kwenye mahema kutokana na ghasia za kisiasa
Familia zinaishi kwenye mahema kutokana na ghasia za kisiasa

Watu wamepatiwa makazi ya muda katika Protection of Civilians katika mji wa malakar tangu mzozo ulipozuka katika eneo mwezi Disemba mwaka 2013. Idadi ya watu wasiokuwa na makazi imeongezeka kufikia 40,000 kufuatia mmiminiko wa watu 10,000 waliokoseshwa makazi mwezi April mwaka 2015 na zaidi ya watu 16,000 waliokoseshwa makazi mwezi Julai na Agosti mwaka jana.

Wengi wanakuja kutoka maeneo ambayo hayakupata msaada kwa miezi kadhaa wanawasili bila vifaa vyovyote.

XS
SM
MD
LG