Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:54

Watu sita wauwawa uwanja wa ndege wa Mogadishu


SOMALIA EXPLOSION
SOMALIA EXPLOSION

Polisi wa Somalia wanasema watu sita wameuwawa Jumatano baada ya watu wawili waliokuwa na bunduki kuushambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu, ambao una ulinzi mkali sana.

Waliofariki dunia ni pamoja na raia mmoja wa Somalia, na watano ni raia kutoka mataifa ya nje.

Watu hao wawili waliuwawa na vikosi vya usalama kwa mujibu wa msemaji wa polisi Meja Abdifatah Aden Hassan.

Amesema mmoja wa raia wa kigeni aliyeuwawa ni mwanajeshi katika tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani AMISOM.

Amesema wengine wanne walikuwa wakufunzi wakiisaidia serekali ya Somalia kujifunza kuhusu masuala ya milipuko.

Kundi la kigaidi la Al Shabab limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

Hassan ameiambia VOA kwamba watu wawili waliokuwa na bunduki walishambulia lango la kuingilia uwanja wa ndege Jumatano mchana na walikabiliwa na vikosi vya usalama.

Uwanja huo wa ndege ndipo yalipo makao makuu ya AMISOM, na pia kuhudumia wanadiplomasia wengi wa kimataifa waliopo Mogadishu.

Mashuhuda wanasema maafisa wa usalama wamesema mashambulizi ya kufyatuliana risasi yalitokea upande wa mashariki wa uwanja wa ndege ambapo kuna maduka mengi.

XS
SM
MD
LG