Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:56

Watu sita wauwawa Darfur


Magari ya UN yakisambaza msaada wa maji huko Darfur
Magari ya UN yakisambaza msaada wa maji huko Darfur

Watu sita wameuwawa katika mkoa wa Darfur wenye matatizo nchini Sudan wakati wa maandamano dhidi ya ongezeko la bei.

Maafisa wa serikali wanasema vifo vilitokea jumanne katika mji mkuu wa kieneo wa Nyala, lakini hawakusema namna vifo hivyo vilivyotokea.watu kadhaa walijeruhiwa.

Awali mashahidi walisema polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi kwa waandamanaji ambao walichoma matairi na kutoa wito wa kuanguka kwa utawala. Ghasia za maandamano ya kupinga serikali kote sudan zimekuwa zikifanyika tangu mwezi uliopita.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jumanne liliongeza mamlaka ya walinda amani katika mkoa wa Darfur kwa mwaka mmoja mwingine, lakini itapunguza idadi ya wanajeshi.

XS
SM
MD
LG