Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:01

Watu nane wapoteza maisha katika dhoruba ya theluji Japan


Theluji iliyokumba Japan .
Theluji iliyokumba Japan .

Theluji kubwa imenyesha kaskazini na magharibi mwa Japan na kuwachochea maafisa wa hali ya hewa kuwataka wakaazi kuwa katika hali ya tahadhari kwa ajhili ya dhoruba ya majira ya baridi Ijumaa.

Theluji imeendelea kunyesha kwenye pwani katika bahari ya Japan kwenye maeneo ya kaskazini na magharibi katika nchi hiyo tangu Desemba 17 na kuua watu wanane na kujeruhi wengine dazeni hadi ilipofika Ijumaa asubuhi, kwa mujibu wa kituo cha umma cha utangazaji nchini Japan, NHK.

Maeneo ya vijijini huko Hokkaido Japan yameshuhudia mita 1 na sentimita 61 za theluji. Kituo cha treni cha Sapporo nchini Japan kimesema kitasitisha safari za treni zinazounganisha mji mkuu wa Hokkaido wa Sapporo.

Maafisa wa hali ya hewa wamewataka wakazi kuwa katika tahadhari kubwa na kutofanya shughuli zozote nje ya nyumba mpaka Jumatatu Desemba 26 wakati theluji kubwa sana huenda ikavuruga usafiri na kusababisha umeme kukatika.

XS
SM
MD
LG