Wimbi la matope huko Casamicciola Terme mojawapo ya miji sita katika kisiwa cha Ischia, yamesababisha uharibifu katika nyumba moja na kusukuma magari kadhaa hadi kwenye bahari.
Watu wawili waliokuwa kwenye moja ya gari hilo wameripotiwa kuokolewa. Taarifa za mapema leo zinasema kuwa watu 13 hawajulikani walipo ikiwemo mtoto mchanga.
Maafisa wamewaomba wakaazi wanaosihi katika maeneo jirani kwenye miji , lakini hawajaathiriwa na maporomoko ya ardhi kubaki nyumbani ili kuepuka kuvuruga juhudi za uokozi zinazoendelea.
Wafanyakazi wa msaada kutoka Naples wamepelekwa kwenye kisiwa hicho lakini hali ya hewa inasababisha ugumu kufikia kisiwa hicho. Mwaka 2017 tetemeko la ardhi Casamicciola Terme liliuwa watu wawili.