Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki ilisema kwenye Twitter mali za watu saba au watu wa kisheria waliohusika katika kufadhili kundi hilo zilizuiwa.
Wizara ya fedha ya Marekani ilisema watu wanne na mashirika mawili ya Uturuki yamewekewa vikwazo.
Miongoni mwao ni raia wa Iraq anayeishi kinyume cha sheria Uturuki, Brukan al-Khatuni, wanawe wawili na washirika wao, na biashara mbili walizotumia kuhamisha pesa kwa niaba ya Islamic State, kati ya Uturuki, Iraqi na Syria.
Wizara ya fedha ya Marekani ilisema katika taarifa yake.
Facebook Forum