Kati ya waliouawa ni mtoto wa kike na mwanamke.
Watu wengine ambao idadi yao haijatajwa, wakiwemo maafisa wa usalama, wamejeruhiwa.
Katika shambulizi ljngine, maafisa wawili wa kijeshi wamepigwa risasai na kuuawa katika mji wa Isfahan, nchini humo.
Shirika la habari la serikali ya Iran limeripoti kwamba waliotekeleza mashambulizi yote mawili walikuwa wanatumia usafiri wa pikipiki.
Haijabainika kilichopelekea mashambulizi hayo ama kama yanahusiana na maandamano yanayoendelea kote nchini Iran kwa muda wa miezi miwili sasa.
Makundi ya waandamanaji yalikuwa yamekusanyika katika sehemu tofauti za Izeh, wakipaaza sauti zenye ujumbe wa kupinga serikali, na kurushia polisi mawe, huku polisi wakitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.