Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 06:19

Watu 95 wameuwawa Mali kwa shambulizi la risasi na nyumba kuchomwa moto


Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita akikagua uharibifu baada ya shambulizi la Machi 25 mwaka huu huko Ogossagou
Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita akikagua uharibifu baada ya shambulizi la Machi 25 mwaka huu huko Ogossagou

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alisikitishwa na shambulizi hilo na alitoa wito kwa pande zote huko Mali kuonesha hatua za kudhibiti ghasia za visasi, kulingana na taarifa iliyoelezwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric

Watu takribani 95 waliuwawa huko kati kati ya Mali siku ya Jumatatu wakati watu wenye silaha waliposhambulia kijiji kimoja usiku kucha na kuwafyatulia watu risasi pamoja na kuchoma moto nyumba zao. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Mali, Amadou Sangho alieleza kwamba angalau watu 19 hawajulikani walipo.

Mwandishi mmoja karika eneo aliiambia Sauti ya Amerika kwamba shambulizi lililenga kijiji cha Sobanetou karibu na kati kati ya mji wa Mopti. Aliendelea kueleza kwamba idadi ya vifo huwenda ikaongezeka na kuvuka 100. Ripoti za awali zilieleza kwamba kijiji hicho wanachoishi watu wenye asili ya Dogon kilionekana kushambuliwa na wapiganaji wenye asili ya Fulani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alisikitishwa na shambulizi hilo na alitoa wito kwa pande zote huko Mali kuonesha hatua za kudhibiti ghasia za visasi, kulingana na taarifa iliyoelezwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric.

Mkulima kutoka kabila la Fulani nchini Mali
Mkulima kutoka kabila la Fulani nchini Mali

Mivutano imekuwepo nchini humo kwa miaka kadhaa kati ya wakulima wa kabila la Dogon na wafugaji wa kabila la Fulani. Machi 23 takribani watu 160 wa kabila la Fulani waliuwawa wakati watu wenye silaha waliposhambulia kijiji cha Ogossagou katika eneo hilo hilo. Wakulima wa kabila la Dogon walishutumiwa kufanya shambulizi hilo.

Mjumbe katika kundi linaloangalia matatizo ya kimataifa, Jean-Herve Jezequel aliandika katika ripoti baada ya mauaji ya mwezi Machi kwamba wakulima hao wamekuwa kundi la wanamgambo wenye silaha wakieleza kwamba wanahitaji kuilinda jamii yao kama vikosi vya usalama vya Mali haviwezi kufanya hivyo.

Alieleza kwenye ripoti hiyo kwamba kuwepo silaha za vita na nia ya wapiganaji wa makundi ya jihadi yamefungua milango ya viwango tofauti vya ghasia zinazohusu makabila.

XS
SM
MD
LG