Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 24, 2025 Local time: 20:01

Watu 8 wauwawa na 7 kujeruhiwa kwa risasi Texas 

Afisa wa Polisi anatembea watu wakiondolewa kutoka kwa kituo cha ununuzi ambapo ufyatuaji risasi ulitokea Mei 6, 2023, huko Allen, Texas.
Afisa wa Polisi anatembea watu wakiondolewa kutoka kwa kituo cha ununuzi ambapo ufyatuaji risasi ulitokea Mei 6, 2023, huko Allen, Texas.

Mtu mmoja mwenye silaha alifyatua risasi kwenye eneo la maduka mengi karibu na Dallas, Texas, na kuua watu wanane na kujeruhi saba Jumamosi, kulingana na mamlaka. 

Mtu mmoja mwenye silaha alifyatua risasi kwenye eneo la maduka mengi karibu na Dallas, Texas, na kuua watu wanane na kujeruhi saba Jumamosi, kulingana na mamlaka.

Maafisa wanasema mtu huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa Polisi ambaye alikuwa katika eneo la maduka liitwalo Allen Premium Outlets.

Polisi bado hawajatoa taarifa kuhusu utambulisho wa waathiriwa au mshukiwa. Hata hivyo, watoto wanaaminika kuwa miongoni mwa waathiriwa, kulingana na watu waliotoka kwenye duka hilo baadaye.

Tukio la Jumamosi ni la hivi punde zaidi katika matukio ya ufyatuaji risasi wa watu wengi mwaka huu. Yanafanyika kwa kiwango cha takriban moja kwa wiki, kulingana na hifadhi data ya shirika la habari la Associated Press na USA Today kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Northeastern.

XS
SM
MD
LG