Maafisa wamesema zaidi ya watu 150 walikuwa kwenye daraja hilo kwenye Mto Machhu katika mji wa Morbi wakati wa kuporomoka.
Picha za runinga zilionyesha dazeni ya watu wakiwa wameng'ang'ania nyaya na mabaki yaliyopinda ya daraja lililoporomoka huku timu za dharura zikijitahidi kuwaokoa. Baadhi walipanda juu ya daraja hilo lililovunjika ili kujaribu kuelekea kwenye kingo za mto, huku wengine wakiogelea hadi sehemu salama.
Vifo sitini vimethibitishwa hadi sasa,"mbunge Mohan Kundariya alisema.
Takriban watu 30 pia wamejeruhiwa, maafisa wengine walisema.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Harsh Sanghavi alisema zaidi ya watu 150 walikuwa kwenye daraja jembamba lililowekwa nyaya, kivutio cha watalii ambacho kilivutia watazamaji wengi wakati wa msimu wa sikukuu, wakati Diwali na Chhath Puja zinasherehekewa.