Dhoruba ya kitropiki Nalgae imeua watu wasiopungua 45 nchini Ufilipino. Mapema Jumamosi, shirika linalofuatilia majanga nchini humo lilisema kimbunga hicho kilisababisha vifo vya watu 72, lakini idadi hiyo ilipungua baada ya kukaguliwa na wafanyakazi katika eneo kwenye mikoa ya kusini na mashariki mwa nchi.
Wataalamu wa hali ya hewa walisema Nalgae, iliyokuwa na upepo wa kilomita 95 kwa saa, na upepo wa hadi kilomita 130 kwa saa, ulisababisha maporomoko mengi ya ardhi kwenye eneo la mashariki mwa Ufilipino.
Wakaazi wameshauriwa kuwa mafuriko na maporomoko ya ardhi yanaweza kutokea baada ya mvua kubwa ya Nalgae.
Meya wa Manila amefunga maeneo yote yenye makaburi kwenye jiji hilo kwa sababu Nalgae inakaribia wakati Wafilipino walipokuwa wanajitayarisha kuadhimisha “Siku ya Watakatifu Wote”-ALL SAINTS DAY kwa utamaduni wa kutembelea makaburi ya jamaa zao.