Makundi ya haki za binadamu huko Syria yanasema majeshi ya usalama yamefyatua risasi dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali katika mji wa Hama na kuuwa watu 27.
Wanaharakati wanasema tukio hilo lilitokea baada ya maelfu ya waandamanaji kuingia mitaani baada ya sala ya Ijumaa katika mji ambao uko kiasi cha kilometa 300 kaskazini mwa Damascus.
Waandamanji walijaa nchi nzima ya Syria Ijumaa kwa majibu ya wito wa makundi ya upinzani ya kuandamana dhidi ya kujeruhiwa watoto katika wiki za karibuni dhidi ya rais Bashar Al Assad.