Zaidi ya watu 20 walijeruhiwa katika ajali hiyo ambayo ilitokea karibu na Sakal eneo la Louga, Papa Ange Michel Diatta, kanali anayefanya kazi na idara ya kitaifa ya zima moto ameiambia AFP.
Waziri mkuu Amadou Ba alilitembelea eneo la ajali akiapa kuimarisha sheria mpya za barabarani.
Basi hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 32 lakini lilikuwa limebeba watu 47, Ba aliwaambia waandishi wa habari, akisema kutoheshimu sheria za barabarani kunaongeza idadi ya vifo.
Rais Macky Sall aliandika kwenye Twitter” Ajali nyingine mbaya kwenye barabara zetu.”
Ameongeza kuwa idadi hiyo ya vifo inaonyesha umuhimu wa kuimarisha sheria za usalama wa barabarani.
Ajali za barabarani ni jambo la kawaida nchini Senegal, hasa kutokana na uzembe wa madereva, barabara mbovu na uchakavu wa magari, wataalam wanasema.
Senegal iliingia kwenye siku tatu za maombolezo baada ya mabasi mawili kugongana mapema asubuhi tarehe 8 Januari katika eneo la katikati la Kaffrine, na kusababisha vifo vya watu 40 na zaidi ya 100 kujeruhiwa.