Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 03:38

Watu 20 wauawa katika mashambulizi Ituri - DRC


Wanajeshi wa DRC katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu waliwauwa takriban watu 20 katika mashambulizi kwenye  vijiji viwili mashariki mwa Congo mwishoni mwa wiki, jeshi na kundi la kutetea haki za binadamu lilisema Jumapili.

Wapiganaji wanaoaminika kutoka kundi la Allied Democratic Forces (ADF) waliwaua wakazi na kuchoma nyumba katika vijiji vya Kandoyi na Bandiboli kwenye jimbo la Ituri Ijumaa na mapema Jumamosi, alisema Christophe Munyanderu, mratibu wa kikundi cha ndani cha Convention for the Respect of Human Rights. (CRDH).

Msemaji wa jeshi la Congo huko Ituri, Jules Ngongo, alithibitisha vifo takriban 20, na kusema kuwa vikosi vya Congo vilikuwa vinawasaka washambuliaji hao.

Ni ngumu sana kwangu nilipoiona miili hiyo, makoo yao yalikuwa yamekatwa,” alisema Alice Kyanga, ambaye wazazi wake walikuwa miongoni mwa waliouawa nyumbani kwao siku ya Jumamosi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG