Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 04:22

Watu 16 wameuawa katika shambulio kaskazini mwa Nigeria


Ramani ya Nigeria na majimbo yake ikiwemo Plateau.
Ramani ya Nigeria na majimbo yake ikiwemo Plateau.

Eneo lililotokea shambulio hilo liko kwenye mstari unaoligawa eneo kati ya Waislam walio wengi huko kaskazini na Wakristo wa kusini nchini Nigeria, kwa miaka mingi wamekuwa wakikabiliwa na mivutano ya kikabila na kidini.

Watu 16 wameuawa katika shambulio huko kaskazini mwa Nigeria ambako mapigano kati ya wafugaji na wakulima ni ya kawaida, jeshi limesema Jumapili. Shambulio hilo lilitokea usiku wa manane Jumamosi katika kijiji cha Mushu kwenye jimbo la Plateau, Kapteni Oya James aliliambia shirika la habari la AFP.

Eneo hilo liko kwenye mstari unaoligawa eneo kati ya waislam walio wengi huko kaskazini na Wakristo wa kusini nchini Nigeria, kwa miaka mingi wamekuwa wakikabiliwa na mivutano ya kikabila na kidini. Haikufahamika mara moja kile kilichosababisha shambulio hilo la hivi karibuni na nani aliyehusika.

Maafisa wa usalama walipelekwa kuzuia mapigano zaidi katika eneo hilo, ambapo mauaji ya kulipiza kisasi, kati ya wafugaji ambao mara nyingi ni Waislamu, na wakulima ambao kwa ujumla ni Wakristo, mara nyingi hugeuka kuwa mashambulizi ya kijiji yanayofanywa na magenge yenye silaha.

Gavana wa jimbo Caleb Mutfwang amelaani shambulio hilo la hivi karibuni kuwa la kikatili, na halikuwa na maana na kuapa kuwafikisha wahusika katika vyombo vya sheria, msemaji wake Gyang Bere, aliwaambia waandishi wa habari.

Forum

XS
SM
MD
LG