Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 16:13

Watu 12 wameshikiliwa Iran kwa tuhuma za kuhujumu uchumi


Ramani ya Iran
Ramani ya Iran

Ghasia za mitaani zilizuka katikati ya mwezi Septemba baada ya kifo cha Mahsa Amini mwanamke mwenye umri wa miaka 22 raia wa Iran mwenye asili ya Kikurdi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa maadili mjini Tehran

Jeshi la walinzi wa Mapinduzi la Iran limewakamata watu 12 wanaodaiwa kuwa wanachama wa kundi lenye uhusiano na Ulaya linalotuhumiwa kupanga vitendo vya kuhujumu uchumi nchini humo shirika la habari la Tasnim limesema.

Jamhuri hiyo ya Kiislamu imetikiswa na zaidi ya miezi miwili ya kile inachokiita "ghasia" mbaya ambazo inasema zimechochewa na Marekani, washirika wake na makundi ya upinzani yenye makao yake makuu nchi za kigeni.

Ghasia za mitaani zilizuka katikati ya mwezi Septemba baada ya kifo cha Mahsa Amini mwanamke mwenye umri wa miaka 22 raia wa Iran mwenye asili ya Kikurdi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa maadili mjini Tehran.

Katika taarifa iliyonukuliwa na Tasnim, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkoa wa Markazi, kusini magharibi mwa Tehran, limesema limekamata "mtandao wenye wanachama 12 wenye uhusiano nje ya nchi".

Ilidai kuwa walikuwa "chini ya uongozi wa mawakala wa kupambana na mapinduzi wanaoishi Ujerumani na Uholanzi" na walifanya "shughuli dhidi ya usalama wa taifa".

XS
SM
MD
LG