Mkurugenzi mkuu wa UNICEF, Catherine Russel, ameuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watoto wa Haiti kwamba wanakadiria kuwa watoto wanachukuwa zaidi ya asilimia 50 ya wanachama wa magenge yenye silaha huku jumla ua idadi ya watoto wanao andikishwa na makundi hayo yameongezeka na kufikia asilimia 70 katika mwaka uliopita.
Ameongeza kusema wanatumika kama watoa taarifa, wapishi, watumwa wa ngono, na wanalazimishwa kuanzisha ghasia miongoni mwao.
Amesema magenge kwa kawaida huwauwa watoto na kwamba matukio ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto yameongezeka maradufu mwaka huu kwa asilimia 1,000.
Forum