Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:44

Watoto wawili wauwawa kwa mlipuko Kashmir


Watoto wawili wameuawa, na raia wengine watano kujeruhiwa katika mlipuko eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India Jumatatu.

Tukio hilo limetokea siku moja baada ya washambuliaji kufyatua risasi kwenye nyumba kadhaa, na kusababisha vifo vya watu wanne, polisi walisema.

Mlipuko huo ulitokea karibu na moja ya nyumba zilizolengwa usiku kucha katika kijiji cha Dhangri, wilayani Rajouri kusini.

Mtoto wa kiume wa miaka 5 na msichana wa miaka 12 walikufa katika mlipuko huo.

Siku ya Jumapili usiku, watu wawili wenye silaha walifyatua risasi katika nyumba tatu huko Dhangri, afisa mkuu wa polisi Mukesh Singh aliwaambia waandishi wa habari.

Polisi wamewashuku wanamgambo wanaopigana na utawala wa India kufanya mashambulizi hayo mawili.

XS
SM
MD
LG