Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 21:02

Watoto wasiotimia umri wa kuzaliwa waondolewa kutoka hospilati ya Gaza


Picha ya watoto walioondolewa kutoka hospitali ya Shifa, Gaza.
Picha ya watoto walioondolewa kutoka hospitali ya Shifa, Gaza.

Maafisa wa afya wa Umoja wa Mataifa wamesema Jumatatu kwamba watoto 31 ambao muda wao wa kuzaliwa ulikuwa haujatimia wameondolewa kutoka kwenye hospitali ya Shifa huko Gaza na kupelekwa Misri kwa ajili ya matibabu. 

Tony Fricker afisa kutoka shirika la watoto la Umoja huo, UNICEF ameambia shirika la habari la utangazaji la BBC, kwamba zoezi hilo la Jumapili lilikuwa gumu sana na lenye hatari kubwa. Ameongeza kusema kwamba hiyo ilikuwa moja ya hatua chache za kutia moyo ndani ya saa 48 zenye changamoto nyingi.

Daktari mmoja kwenye hospitali ya kusini mwa Gaza walikopelekwa watoto hao amekiambia kituo cha televisheni cha CNN kwamba hali yao ni nzuri, lakini ngumu. Amongeza kusema kwamba hali yao huenda ikadorora wakati wowote.

Timu za maafisa wa afya za Misri zinasubiri kupokea watoto hao kwenye kivuko cha mpakani cha Rafah. Jumapili Israel imeonyesha video iliyoonyesha handaki lililochimbwa na wanamgambo wa Hamas chini ya hospitali ya Shifa, wakati ikiendelea kuwasaka na kuwaangamiza wanamgambo wa hao.

Forum

XS
SM
MD
LG