Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:37

Watoto wachanga wafariki kutokana na ajali ya moto hospitalini, Senegal


Mama wa mtoto mwenye umri wa siku 10aliyefariki katika ajali ya moto iliyotokea katika hospitali ya Tivaouane, Senegal, May 26, 2022.
Mama wa mtoto mwenye umri wa siku 10aliyefariki katika ajali ya moto iliyotokea katika hospitali ya Tivaouane, Senegal, May 26, 2022.

Rais wa Senegal Macky Sall, amesema kwamba watoto wachanga 11 waliozaliwa katika hospitali ya Watoto mjini Tivawane, wamefariki kutokana na moto.

Katika ujumbe wa twiter, rais Sall amesema kwamba amesikitika kutokan ana tukio hilo na kuwaonea huruma mama na familia za watoto hao.

Maafisa wamesema kwamba hitilafu ya nguvu za umeme ndio umesababisha moto huo katika hospitali ya Mame Abdou Aziz Sy Dabakh mjini Tivawane, uliyo umbali wa kilomita 120 kutoka mji mkuu wa Dakar.

Tukio hilo limejiri mwaka mmoja baada ya watoto wachanga kufariki kutokana na tukio la moto katika mji wa Linguere, kaskazini mwa Senegal.

Vifo kadhaa vya watoto wachanga vimetokea katika siku za hivi karibuni na kusababisha wasiwasi kuhusu mfumo wa afya ya watoto katika nchi hiyo ya Afrika magharibi inayotambulika kuwa na hospitali bora zaidi katika eneo hilo.

Mapema mwezi huu, maafisa waligundua mtoto aliyekuwa hai akiwa amewekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti, Mtoto huo alifariki baadaye.

XS
SM
MD
LG