Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 07:07

Watoto wa Joseph Kony wawekewa vikwazo na Marekani


Wizara ya hazina ya Marekani imeweka vikwazo vya kifedha dhidi ya watoto wawili wa kiume wa Joseph Kony, kiongozi wa kundi la Lord’s Resistance Army (LRA) ambalo ni kundi linalopigana vita vya umwagaji damu huko Afrika ya Kati.

Hazina Jumanne imezuia mali zao zote zilizopo Marekani za Salim na Ali Kony na kukataza Wamarekani kufanya nao biashara.

Vikwazo kama hivyo viliwekwa kwa Joseph Kony mwezi Machi mwaka huu.

Salim na Ali Kony wapo katika uongozi wa kundi la LRA toka mwaka 2010.

Ali anatarajiwa kuchukuwa nafasi ya baba yake katika kundi hilo la uasi kutoka Uganda, na wote wawili wanahusika na kusimamia nidhamu ndani ya kundi.

Maafisa wa hazina ya Marekani wansema Salim anashutumiwa kufanya mauaji ya wanachama LRA ambao walitaka kuondoka katika kundi hilo la wanamgambo.

XS
SM
MD
LG