Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 19:53

Watoto 80 waliokamatwa nchini Chad wamepewa dhamana


Hali ya kisiasa nchini Chad
Hali ya kisiasa nchini Chad

Maandamano yaliyopigwa marufuku yalifanyika Oktoba 20 kuadhimisha tarehe ambayo awali jeshi lilikuwa limeahidi kukabidhi madaraka ratiba ambayo sasa imeongezwa kwa miaka miwili

Watoto 80 ambao walikamatwa na kuzuiliwa katika gereza la jangwani kufuatia maandamano mabaya nchini Chad mwezi Oktoba wamepewa dhamana, mwendesha mashtaka wa umma Moussa Wade Djibrine alisema Alhamisi.

"Ombi la wao kuachiliwa kwa muda liliwasilishwa na hakimu alikubali," alisema, akiongeza kuwa kesi dhidi ya watoto hao bado "inaendelea."

Mamia ya watu walikamatwa kufuatia maandamano ya umwagaji damu dhidi ya utawala wa Chad, ambapo watu 262 wamehukumiwa kifungo cha hadi miaka mitatu.

Maandamano yaliyopigwa marufuku yalifanyika Oktoba 20 kuadhimisha tarehe ambayo awali jeshi liliahidi kukabidhi madaraka ratiba ambayo sasa imeongezwa kwa miaka miwili.

Maandamano yaliyopigwa marufuku yalifanyika Oktoba 20 kuadhimisha tarehe ambayo awali jeshi lilikuwa limeahidi kukabidhi madaraka ratiba ambayo sasa imeongezwa kwa miaka miwili.

Takriban watu 50 walifariki, wakiwemo maafisa 10 wa vikosi vya usalama, kulingana na idadi rasmi.

XS
SM
MD
LG