Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 22:16

Watawa watekwa Nigeria


Taasisi moja ya kidini mapema Jumatatu imesema watawa wanne wa kikatoloki wametekwa katika barabara kuu ya Nigeria, katika jimbo linalo zalisha mafuta la kusini mashariki.

Watawa hao walikuwa njiani kwenda kuhudhuria ibada.

Taasisi ya kidini ya Sisters of Jesus the Savior, imesema katika taarifa yake kwamba watawa hao walitekwa Jumapili katika eneo la Okigwe-Umulolo.

Taarifa imeeleza zaidi kwamba wanaendelea na maombi makubwa ili waweze kuachiwa kwa haraka.

Taasisi hiyo katika mtandao wake inasema watawa hao “wanaomba mwenyezi mungu awasimamie katika kila jambo."

Katika upande wa kaskzini magharibi jeshi limeanza mashambulizi ya anga kuondoa makundi ya wenye silaha yanayo husika kwa kuteka raia kutoka katika vijiji na mii ya eneo hilo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG