Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 06:15

Watanzania wamsubiri rais Obama leo Jumatatu


 Rais Barack Obama na mkewe Michele Obama
Rais Barack Obama na mkewe Michele Obama
Rais wa Marekani Barack Obama ataendelea kuelezea azma ya Marekani ya kuwa na ushirika wa wenye nguvu wa kibiashara baina ya nchi yake na bara la Afrika atakapowasili Tanzania Jumatatu Alasiri, kituo chake cha mwisho katika ziara ya nchi tatu barani humo.

Rais Obama atashiriki katika mkutano na wafanyabiashara leo Jumatatu mjini Dar es Salaam kusikiliza maoni ya wakurugenzi wakuu wa mashirika ya kibiashara na viongozi kutoka Afrika na Marekani.

White House inasema mkutano huo utashirikisha wawakilishi kutoka makampuni ya Marekani ya Coca- Cola, General Electric na Microsoft, na utahudhuriwa pia na wawakilishi wa benki ya Equity kutoka Kenya na Econnect Telecommunications ya Zimbabwe, miongoni mwa wengine.

Rais wa Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB ) Donald Kaberuka pia atawakilisha benki hiyo kwenye kikao hicho cha pamoja. Kaberuka aliiambia Sauti ya Amerika kuwa benki hiyo inakaribisha ziara ya rais wa Marekani na juhudi zake za kuunga mkono uwekezaji wa sekta binafsi ya Marekani katika Afrika. Benki ya Maendeleo ya Afrika inashirikiana na Marekani katika mradi mpya uliozinduliwa na rais Obama wa kuimarisha huduma za nishati barani humo.

Mpango huo unajulikana kama “Power Africa” na utagharimu dola bilioni 8 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.Mpango huo pia unalenga kuimarisha huduma za umeme katika nchi sita za Kenya, Tanzania, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Liberia.

Kabla ya kikao hicho cha wafanyabiashara, rais Obama atafanya mazungumzo na rais wa Tanzania Jakaya Kikwete. Tanzania hupokea misaada mingi kutoka Marekani. Mingi inatoka kwenye mfuko wa dola milioni 700 za malengo ya milinia kwa lengo la kuimarisha miundo mbinu yake.
XS
SM
MD
LG