Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 23:12

Watano wafa kutokana na bomu Somalia


Wanajeshi wa Somalia wakilinda miili ya magaidi waliokufa kutokana na shambulizi la kigaidi , Picha ya maktaba
Wanajeshi wa Somalia wakilinda miili ya magaidi waliokufa kutokana na shambulizi la kigaidi , Picha ya maktaba

Polisi pamoja na mashuhuda nchini  Somalia wamesema kwamba bomu lenye nguvu la kwenye gari Jumapili limeua takriban watu watano nje ya mgahawa maarufu katikati mwa nchi. 

Wanamgambo wenye uhusiano na kundi la kigaidi la al Qaida wamedai kuhusika na sh,ambulizi hilo. Mlipuko huo pia umewajeruhi watu wengine 14 pamoja na kuharibu majengo mengine karibu na mgahawa huo kwenye mji wa Jowhar ulioko takriban kilomita 90 kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, washambuliaji waliendesha gari lililojaa vilipuzi kwenye ukuta wa mgahawa wa Nur-doop, ambao ni maarufu sana miongoni mwa wabunge pamoja na maafisa wa serikali. Afisa wa usalama Mohamed Ali kutoka mjini humo alisema kwamba miongoni mwa watu waliokufa ni wanawake waliokuwa wakifanya kazi kwenye mgahawa huo.

Waziri mkuu mpya Hamza Abdi Barre aliyeidhinishwa na bunge mwezi Juni ametuma salaam za rambi rambi kwa waathirika huku akiahidi msaada wa serikali kwa wale waliojeruhiwa kwenye mkasa huo.

XS
SM
MD
LG