Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 06:01

Watafiti Marekani wanafanya uchunguzi zaidi wa kugundua Alzheimer


Ubongo wenye afya usiokuwa na Alzheimer (L) na ubongo uliokuwa na Alzheimer (R).
Ubongo wenye afya usiokuwa na Alzheimer (L) na ubongo uliokuwa na Alzheimer (R).

Watafiti wa vyuo vikuu nchini Marekani walisema wamefanya uchunguzi wa damu ambao unaonekana kugundua hatua za awali za ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu-Alzheimer ambao ni sababu kubwa kwa wazee kupoteza kumbukumbu.

Wanasayansi kwenye chuo kikuu cha Rowan katika jimbo la mashariki la New Jersey walisema majaribio yao ya damu yanaweza kugundua sehemu ya ugonjwa huo ambao unaonekana kwa wagonjwa miaka 10 au zaidi kabla dalili mbaya hazijasambaa za ugonjwa wa Alzheimer ambazo hupelekea kifo.

Sio kila mmoja mwenye hatua za awali za ugonjwa anapata Alzheimer na hali ijulikanayo kama MCI inaweza kusababishwa kwa kiasi kikubwa na sababu mbali mbali ikiwemo ugonjwa wa MS, Parkinson, matatizo ya misuli, msongo wa mawazo na majeraha ya ubongo.

Watafiti wa Rowan walioandika katika jarida la Alzheimer’s Association walisema uchunguzi wao wa damu unaweza kutofautisha kati ya ukuaji tofauti wa hatua za awali na kutambua kwa takribani asilimia 100 ya chembe chembe ambazo zinaonekana kuwa na mafanikio ya kukuza Alzheimer.

XS
SM
MD
LG