Jopo la kimataifa la wataalam limekosoa vikali jinsi mlipuko wa Ebola ulivyodhibitiwa Afrika magharibi miaka miwili iliopita.
Wataalam hao wamependekeza marekebisho ya kuimarisha mifumo ya kitaifa na kimataifa ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko katika siku zijazo.
Jopo hilo limesema kuwa Guinea wala Sierra Leone hazikuwa na uwezo wa kukabiliana na mlipuko huo na pia misaada ya kimataifa haikuwa ya kutosha.
Kiongozi wa Jopo hilo Suerie Moon kutoka chuo kikuu cha Havard amesema wanasayansi na wafanyakazi wa afya hawakuwa na habari za kisasa kuhusu ugonjwa huo ulivyokuwa ukienea miongoni mwa changamoto zingine.
Theluthi moja ya mapendekezo hayo ni kuimarishwa kwa mfumo wa kimataifa wa afya kama kuhusisha baraza la usalama la umoja wa mataifa kwenye maswala ya afya.