Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:49

Waasi wa M23 wapigana na jeshi la DRC


Waasi wa M23 katika mji wa Kiwanja, Aug. 4, 2013.
Waasi wa M23 katika mji wa Kiwanja, Aug. 4, 2013.
Vikosi vya serikali ya Congo na wapiganaji waasi wamepambana vikali katika siku ya tano ya mapigano mashariki mwa mji wa Goma.

Daktari mmoja aliyekuwa mstari wa mbele katika mapigano hayo amesema huduma za afya zimepata changamoto kubwa kutokana na majeruhi wengi. Mapigano baina ya jeshi la serikali na kundi la waasi wa M23 yalidumu usiku kucha kuanzia Jumamosi hadi Jumapili huko Mujoga takriban kilomita 17 kaskazini mwa Goma.

Daktari Isaac Warwanamiza ameiambia Sauti ya Amerika kwa njia ya simu alikuwa hospitali pamoja na Watanzania walioko katika jeshi la Umoja wa Mataifa wakisubiri kwenda mstari wa mbele na kwamba wote waliomzunguuka waliuawa na wengine wengi ni majeruhi.Alisema kufikia Jumapili asubuhi watu 82 walikuwa wameuawa.

Wakati, huo, huo Marekani imesema imeshtushwa na ghasia zinazoendelea baina ya kundi la M23 na jeshi la FARDC mashariki mwa Congo. Katika taarifa iliyotolewa Jumapili jioni na wizara ya mambo ya nje ya Marekani ililaani hatua ya waasi wa M23 ya kusababisha majeruhi ya raia na kushambulia tume ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO na kupelekea raia wengi kutoroka manyumbani mwao.
XS
SM
MD
LG