Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:01

Washukiwa wa ISIS wafunguliwa mashtaka Marekani


 Mohaammad Faarah mwenye umri wa miaka 22 anakabiliwa na mashtaka ya kupanga kujiunga na kundi la Islamic State.
Mohaammad Faarah mwenye umri wa miaka 22 anakabiliwa na mashtaka ya kupanga kujiunga na kundi la Islamic State.

Mahakama moja ya serikali kuu ya Marekani inaendelea kusikiliza kesi ya wanaume watatu raia wa Marekani, wenye asili ya Kisomali na ambao wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga kujiunga na kundi la kigaidi la Islamic State. Kesi hiyo inaendelea kwenye mji wa Minnepolis kwa wiki ya pili mfululizo.

Washukiwa hao, Mohammed Farah, mwenye umri wa miaka 22, Guled Omar, mwenye umri wa miaka 21, na Abdirahman Daudi, aliye na umri wa miaka 22, huenda wakakabiliwa na kifungo cha miaka 15 hadi maisha, iwapo watapatikana na hatia ya kupanga njama za kutekeleza mauaji nje ya Marekani. Wote watatu wamekana mashtaka.

Bi Fadumo Hussein, mama yake Guled Omar, aliiambia Sauti ya Amerika kuwa anaamini maafisa wa kijasusi wa FBI waliwagawanya vijana hao watatu na kufanya kila mmoja kumgeuka mwenzake.

XS
SM
MD
LG