Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 06:06

Wasomali 6 wauwawa katika mlipuko wa bomu Somalia.


Askari wa Alshabab wakifanya mazoezi Somalia.

Waandishi wa habari wnusurika na mlipuko huo uliouwa watu 6 mara tu baada ya wao kuondoka katika eneo hilo.

Bomu moja limelipuka katika mji mkuu wa Somalia na kuuwa wasomali 6 wakiwemo maafisa wawili wa Polisi muda mfupi baada ya kundi la waandishi wa kimataifa kuwepo katika eneo hilo.

Maafisa wa Umoja wa mataifa wamesema bomu hilo linaaminika kuwa limetengenezwa nyumbani , linaonekana lilipangwa kuwalenga polisi kwenye kituo cha ukaguzi karibu na eneo lililojaa watu kwenye nyumba za muda za wakimbizi.

Waandishi walitembelea kituo cha kutoa chakula muda mfupi tu karibu na makazi hayo katika ziara iliyofadhiliwa na Umoja wa mataifa kuangalia juhudi za misaada za kimataifa. Ukame na ghasia mbaya zimefanya Somalia kuwa ni moja ya maeneo yenye mzozo mbaya wa kibinaadamu duniani.

XS
SM
MD
LG