Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:44

Wasichana 100 watekwa nyara Nigeria


Wanawake katika hospitali ya Asokoro mjini Abuja wakilia baada ya shambulizi la bomu mjini humo- April 14, 2014.
Wanawake katika hospitali ya Asokoro mjini Abuja wakilia baada ya shambulizi la bomu mjini humo- April 14, 2014.

Watu hao walichoma moto majengo ya sekondari ya wasichana hao kabla ya kuwajaza kwenye gari na kuondoka nao.

Watu wenye silaha na ambao hawakutambuliwa, wamewateka nyara wasichana wasiopungua 100 kutoka shule moja kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Mashahidi wanasema utekaji nyara huo ulifanyika baada ya waasi kushambulia mji wa Chibok ulioko jimbo la Borno Jumatatu usiku.

Mkazi mmoja wa eneo hilo aliiambia Sauti ya Amerika, kwamba watu hao walichoma moto ofisi na shule ya sekondari ya wasichana hao, ambayo ni ya serikali na kisha kuwajaza wanafunzi hao kwenye gari na kuondoka nao.

Ripoti za awali zilisema kiasi cha wasichana 200 walitekwa nyara. Mwandishi wa VOA katika eneo hilo Abdulkareem Haruna anasema vyanzo vya habari kutoka eneo la tukio hilo vinasema kuwa baadhi ya wasichana waliweza kutoroka.
XS
SM
MD
LG