Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 10:09

Washukiwa wengine wa uharamia wakamatwa Kenya


Moja ya meli iliyowahi kutekwa na maharamia wa somalia

Osifi ya mwanasheria mkuu kupitia wakili wa serikali Catherene Mwaniki imeagiza ripoti ya madaktari kuhusu uchunguzi wa umri, wa washukiwa hao wa uharamia.

Washukiwa wengine wanne wa uharamia raia wa Somalia, wanashikiliwa na polisi mjini Mombasa tangu Jumamosi.

Jeshi la Uholanzi liliwakabidhi kwa polisi nchini Kenya ili kufunguliwa mashtaka ya kujaribu kuiteka nyara meli moja ya uvuvi F/V Tahiri kati ya Desemba moja mbili mwaja jana.

Jumatatu wamefikishwa mahakamani Mombasa, mbele ya hakimu mkuu Lilian Mutende, lakini hata kabla ya kusomewa mashtaka wameibua maswala kadhaa ikiwemo kupinga uhalali wa mahakama ya Kenya kuwafungulia mashtaka.

Wakili wao Jared Magolo anasema hawakukamatwa katika maji ya Kenya na kwamba

wao ni vijana wadogo waliokamatwa kimakosa.

Osifi ya mwanasheria mkuu kupitia wakili wa serikali Catherene Mwaniki imeagiza ripoti ya madaktari kuhusu uchunguzi wa umri, wa washukiwa hao wa uharamia.

Jumanne mahakama ya Mombasa itaamua iwapo vijana hao wenye asili ya Kisomali kama watafunguliwa mashtaka rasmi, na polisi ya Kenya.

XS
SM
MD
LG