Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 13, 2025 Local time: 10:30
VOA Direct Packages

Washington kutathmini upya sera zake na utawala wa Taliban wa Afghanistan


Picha ya jengo la bunge la Marekani mjini Washington.
Picha ya jengo la bunge la Marekani mjini Washington.

Baada ya karibu miaka miwili ya mivutano ya kidiplomasia na utawala wa Taliban, Washington inatathmini sera yake kuhusu Afghanistan kutokana na kile maafisa wa Marekani wametaja kuwa utawala kandamizi wa Taliban.

Tadhmini hiyo inakuja wakati Umoja wa Mataifa ukitathmini kusitisha operesheni ndani ya Afghanistan, kutokana na marufuku iliyowekwa na Taliban dhidi ya wanawake kufanya kazi kwenye mashirika ya UN. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ameiambia VOA Jumatano kwamba Marekani imekuwa ikitathmini upya uhusiano wake na Afghanistan kutokana na sheria kandamizi zinazolenga wanawake na wasichana nchini humo.

Licha ya kukosolewa kimataifa hata kutoka kwa baadhi ya mataifa ya kiislamu, Taliban imesisitiza kwamba kuwanyima wanawake haki ya masomo, ajira au kushiriki kwenye siasa, ni suala la ndani la Afghanistan. Hatua ya Washington imetangazwa wakati katibu mkuu wa UN Antonio Guterres akiripotiwa kupanga kikao cha kimataifa mwezi ujao, ili kujadili kuhusu uwezekano wa kutambua Taliban kwenye baraza kuu la Umoja huo, kwa masharti ya kubatilisha sheria kali ilizoweka dhidi ya wanawake wa Afghanistan.

XS
SM
MD
LG