Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:41

Washington ina imani Kyiv itaendelea kutwaa ardhi yake kutoka Russia


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alisema Marekani imedhamiria kuongeza msaada wake kwa Ukraine ili iweze kufanikiwa katika uwanja wa vita. Mfuko wenye faida wa msaada wa kisiasa na vitendo kwa Ukraine, Blinken aliongeza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumatatu kwamba ingawa ilikuwa mapema mno kutabiri ni wapi mashambulio ya Ukraine yanaelekea, Washington ilikuwa na imani kwamba Kyiv itaendelea kutwaa ardhi yake inayokaliwa kwa mabavu na Russia.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Washington siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alisema Marekani imedhamiria kuongeza msaada wake kwa Ukraine ili iweze kufanikiwa katika uwanja wa vita. Mfuko wenye faida wa msaada wa kisiasa na vitendo kwa Ukraine, Blinken aliongeza, pia inaweza kutarajiwa katika mkutano ujao wa NATO huko Vilnius.

Blinken amesema ingawa ni mapema mno kutabiri ni wapi Ukraine itaongoza, Washington ina imani kwamba Kyiv itaendelea kuchukua ardhi yake iliyokaliwa na Russia. Ukraine inasema tangu kuanza kwa mashambulizi yake wiki iliyopita, vikosi vyake vimekomboa vijiji saba kusini- mashariki.

Katika hotuba yake kwa njia ya video ya Jumatatu usiku, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, alibainisha maendeleo ya vikosi vya Ukraine wakati wa vita vikali na licha ya kuwepo hali ya hewa isiyofurahisha. Nguvu ya wapiganaji wetu bado inazaa matokeo, alisema. Zelenskyy alimshukuru kila mtu ambaye yuko vitani sasa, kila mtu anayeunga mkono wanajeshi wetu kupambana katika maeneo husika, aliongeza.

Afisa mmoja wa Ukraine amesema Jumatatu kuwa wanajeshi wa nchi hiyo walichukua udhibiti wa Storozhov, kijiji katika mkoa wa Donetsk kama sehemu ya kukabiliana na mashambulizi hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG