Utawala wa Biden umekuwa wazi, makini, na imara sana katika kurudisha nyuma shughuli za Iran zinazoyumbisha kanda ya Mashariki ya Kati, ikijumuisha maendeleo ya mpango wa makombora ya masafa marefu, alisema John Kirby, mkurugenzi wa mawasiliano ya kijeshi katika Baraza la Usalama la Taifa.
Aliongeza kusema Sitazungumzia kuhusu ripoti maalum za kombora hili linalodaiwa kuwa ni la kwenda kwa kasi, lakini tumeweka vikwazo vya wazi na shughuli nyingine ili kurudisha nyuma kile Iran inafanya katika kanda hiyo, kwa mara nyingine tena, kujumuisha mpango wao wa makombora ya masafa marefu.
Televisheni ya taifa nchini Iran inasema kombora hilo linaloitwa Fattah, lina uwezo wa kwenda umbali wa kilomita 1,400. Hayo ni masafa mafupi tu ya umbali wa angani kati ya Tehran na Jerusalemu. Rais wa Iran, Ebrahim Raisi ameitaja silaha hiyo mpya kama nanga ya usalama wa kudumu na amani katika kanda ya Mashariki ya Kati.
Forum