Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:12

Washambulizi wateketeza hotel Lamu - Kenya


Mlipuko wa bomu ndani ya soko la Gikomba Nairobi May 16 2014
Mlipuko wa bomu ndani ya soko la Gikomba Nairobi May 16 2014
Habari kutoka mji wa Mpeketoni, katika pwani ya kaskazini mashariki ya Kenya zinaeleza kwamba wapiganaji wanaodhaniwa ni wakundi la Al Shabab kutoka Somalia wameshambulia kituo cha polisi na hoteli kadhaa na kusababisha mapigano makali ya saa mbili na polisi wa Kenya.

Mkuu wa polisi wa Mpeketoni, Hamaton Mwaliko ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba washambulizi waliteka lori katika mji wa Wito Jumapili jioni na kulitumia kushambulia mji huo, akisema hawajui idadi ya majeruhi au vifo.

Hata hivyo kuna ripoti za wanajeshi watatu walouliwa lakini hakuna habari huru za kuthibitisha.

Afisa huyo wa polisi anasema, baadhi ya hoteli zimeteketea na washambuliaji walikimbia na maafisa wa jeshi la Kenya wanawafuata.

Kenya imekuwa ikishambuliwa na wapiganaji wa Al Shabab tangu pale serikali ilipowapeleka wanajeshi wake huko Somalia mwaka 2011.
XS
SM
MD
LG