Bajeti imepitishwa licha ya upinzani mkali kutoka kwa maseneta wa chama cha Democratik.
Warepublican wametumia fursa ya kuwa wengi bungeni na kupitisha mswaada huo kwa kura 52 dhidi ya 48.
Wademocrat wote na seneta mmoja wa Republican wamepinga mswaada huo.
Mswaada huo ni sehemu ya bajeti pana inayojumuisha dola trilioni 4.5 kwa ajili ya msamaha wa mabilionea kulipa kodi.
Kuna mswada mwingine unaotayarishwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mike Johnson, wa kupunguza dola trilioni 2 kwa mipango ya afya.
Forum