Warepublican katika Baraza la Wawakilishi wanaelekea kupiga kura, baadaye wiki hii, ambayo itaanzisha uchunguzi unaoendelea wa kumshtaki kumuondoa madarakani Rais Joe Biden.
Lakini bado haijulikani iwapo uongozi huo una kura za kutosha kuidhinisha hatua hiyo. Huku kukiwa na uwezekano wa upigaji kura katika siku chache tu, ukusanyaji maoni mpya uliotolewa Jumatatu asubuhi unaonyesha kuwa idadi ndogo ya Wamarekani wanaamini uchunguzi unapaswa kusonga mbele, lakini hata miongoni mwa Wa-republican wanaojitambua, shauku ya uchunguzi inapungua.
Utafiti huo uliofanywa na kituo cha kukusanya maoni cha Morning Consult, umebaini kuwa asilimia 44 ya Wamarekani wanaamini uchunguzi huo unapaswa kusonga mbele, ikilinganishwa na asilimia 40 ambao wanaamini kuwa haufai.
Matokeo hayo yanadhoofisha kwa kiasi kikubwa msimamo wa chama, huku asilimia 62 ya Wademocrat wakisema uchunguzi huo haupaswi kuendelea, wakati asilimia 70 ya Wa-republican wanasema ni lazima.
Asilimia 47 ya wanaojitegemea walisema uchunguzi huo haupaswi kuendelea, huku asilimia 37 wakisema ni lazima ufanyike.
Forum