Msemaji wa wapiganaji haoGetachew, ameambia shirika la habari la Reuters kwamba ana matumaini kwamba hatua yao itaruhusu msaada wa chakula, ambao unahitajika sana, utaingia Tigray kwa wingi.
Mkuu wa polisi wa Afar Ahmed Harif amesema kwamba wapiganaji hao wameondoka mji wa Abala, lakini bado wapo katika wilaya tatu za eneo hilo.
Amesema kwamba wapiganaji hao wanadhibithi barabara kuu kati ya Abala na mji mkuu wa Tigray wa Mekelle, akiongezea kwamba anaendelea kuzungumza na maafisa wa serikali katika sehemu hiyo pamoja na wapiganaji, wanaompatia taarifa zaidi.