Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:44

Wapalestina wakubaliana kutanzua tofauti zao


Azzam al-Ahmad (kushoto), mkuu wa Fatah, na Mousa Abu Marzook, afisa mwandamizi wa Hamas, wakizungumza na waandishi habari baada ya rais Mahmoud Abbas kutangaza makubaliano mepya.
Azzam al-Ahmad (kushoto), mkuu wa Fatah, na Mousa Abu Marzook, afisa mwandamizi wa Hamas, wakizungumza na waandishi habari baada ya rais Mahmoud Abbas kutangaza makubaliano mepya.

Makundi mawili makuu ya Palestina Fatah na Hamas yameafikiana kuunda serikali ya mpito ya muungano na kutayarisha uchaguzi.

Kundi la Fatah linalotawala Ukingo wa Magharibi na wahasimu wao wanaharakati wa kislamu wa Hamas wanaodhibiti Gaza wamesema walifikia makubaliano hayo wakati wa majadiliano ya siri huko Cairo.

Bila ya kuchelewa Israel imejibu kwa tangazo lililoshtusha wengi, lililotolewa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu kwenye televisheni ya Israel.

Bw Netanyahu anasema rais wa mamlaka ya Wapalestina Mahamoud Abbas analazimika kuchaguwa kati ya amani na Israel au amani na Hamas, ambao anasema wanajaribu kuitokomeza Israel. Kiongozi huyo wa Israel anasema wazo tu la upatanishi, linaonesha udhaifu wa utawala wa Palestina ambao Hamas inaweza kuchukuwa udhibiti wa Ukingo wa Magharibi.

Makubaliano hayo huwenda yakatiwa saini katika siku chache zijazo. Maandamano ya hivi karibuni kwenye Ukingo wa Magharibi na Gaza yamekuwa yakitoa wito wa kukomeshwa ugomvi kati ya makundi hayo mawili.

Wapalestina wengi wanaamini uwongozi ulogawika unawazuia kukabiliana vilivyo na Israel, kumaliza ukaliaji wa ukingo wa magharibi na kuundwa kwa taifa la wapalestina.

Hussam Khader kiongozi wa fatah katika mji wa Nablus huko ukingo wa magharibi anasema,"nina amini itawasaidia wananchi wa Palestina na huwenda itakuwa hatua muhimu kuelekea malengo yetu ya kitaifa".

Hata hivyo kuna shaka ikiwa mkataba utaweza kupelekea upatanishi. Fatah kundi la wastani ambalo limekuwa likijadiliana na Israel. Katiba ya Hamas inataka kuangamizwataifa la wayahudi.

Khader anakumbusha jinsi majaribniyo yaliyopita ya upatanishi yalivyoshindwa na mara nyingine kupelekea ghasia akisema, "tatizo ni kubwa, kubwa mno, na kuna mwanya mkubwa wa kisiasa kati ya Fatah na Hamas, kuhusiana na muelekeo wa vita vya ukombozi".

Makubaliano hayo yaliyofikiwa kupitia upatanishi wa serikali ya mpito ya Misri inayochukuliwa na wapalestina kuwa inaunga mkono zaidi vita vyao kuliko rais aliyepinduliwa Hosni Mubarak.

Lakini Hillel Frisch mtafiti wa cheo cha juu katika kituo cha taaluma ya mikakati ya Begin Sadat karibu na Tel Aviv anahoji ikiwa uungaji mkono wa misri pekee unatosha.

"Hii si taifa la Misri chini ya Mubarak, Hii ni Misri iliyodhaifu.Hakuna aliye na uhakika Misri inaelekea wapi. Ni kweli Misri, kupitia waziri mpya wa mambo ya nchi za nje anazungumza kwa sauti tofauti, sauti ambayo inaunga mkono kwa nguvu wapalestina, lakini taifa linalomuunga mkono ni dhaifu zaidi.

Hamas walishinda viti vingi katika bunge la Palestina 2006. Mwaka ulofuata wanaharakati wa Hamas waliwafukuza Fatah kutoka Ukanda wa Gaza baada ya mapambano mkali ya wiki nzima.

XS
SM
MD
LG