Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:16

Waombolezaji wajitokeza Tokyo kutoa heshima zao za mwisho kwa Abe


Watu watazama jeneza la Abe mjini Tokyo Jumanne
Watu watazama jeneza la Abe mjini Tokyo Jumanne

Waombolezaji nchini Japan Jumanne wametoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.

Raia wa kawaida wamepanga foleni nje ya hekalu la Zojoji mjini Tokyo wakati wakiwa na mashada ya maua pamoja na vifurushi vingine ili kutoa heshima zao. Kabla ya raia kuruhusiwa kuona jeneza lake, ibada maalum iliyohudhuriwa na familia, jamaa na marafiki wa karibu ilifanyika ndani ya hekalu hilo kabla ya kuwekwa kwenye gari maalum la kubebea maiti na kupitishwa kwenye barabara za Tokyo kuelekea kwenye ukumbi wa mazishi wa Kirigaya ili kuchomwa.

Jeneza la Abe limepitishwa kwennye maeneo muhimu kama vile ofisi za waziri mkuu, majengo ya bunge pamoja na makao makuu ya chama chake cha Liberal Demokratik. Abe alipigwa risasi mwishoni mwa wiki wakati akihudhuri mkutano wa kampeni kwenye jimbo la Nara magharibi mwa Japan, na kisha kutangazwa kufa muda mfupi baada ya kukimbizwa hopitalini. Rambi rambi zimeendelea kutolewa na viongozi tofauti wa kimataifa.

XS
SM
MD
LG