Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 02:18

Wanawake Saudia kuanza kuendesha magari 2018


Mwanamke wa Saudia katika kampeni ya kukaidi wanawake kutoendesha magari.
Mwanamke wa Saudia katika kampeni ya kukaidi wanawake kutoendesha magari.

Saudi Arabia itawaruhusu kwa mara ya kwanza wanawake kuendesha magari kwa mujibu wa amri iliyotolewa na mfalme wa nchi hiyo.

Vyombo vya habari vimeripoti Jumanne kuhusu amri hiyo ya kifalme ambayo inataka leseni za kuendesha magari zitolewe kwa wote wanaume na wanawake.

Saudi Arabia hivi sasa ni nchi pekee ambapo inawazuia wanawake kuendesha magari. Shirika la habari la Saudi Arabia -SPA limeripoti kuwa amri hiyo itaanza kutumika rasmi mwezi Juni mwaka 2018.

XS
SM
MD
LG