Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 16:10

Wanawake wa Afghanistan waandamana kupinga kuzuiliwa katika elimu ya juu


Wanawake wa Afghanistan wakiimba nyimbo za kupinga kufungwa kwa vyuo vikuu vya wanawake na Taliban huko Kabul.
Wanawake wa Afghanistan wakiimba nyimbo za kupinga kufungwa kwa vyuo vikuu vya wanawake na Taliban huko Kabul.

Darzeni ya wanawake walionekana wakiandamana barabarani magharibi mwa Kabul siku ya Alhamisi wakipinga marufuku ya utawala unaoongozwa na Taliban.

Darzeni ya wanawake walionekana wakiandamana barabarani magharibi mwa Kabul siku ya Alhamisi wakipinga marufuku ya utawala unaoongozwa na Taliban dhidi ya wanawake kuzuiliwa kwenye elimu ya juu, video iliyotumwa na vyombo vya habari vya ndani ilionyesha.

Uamuzi wa kuwazuia wanawake ulitangazwa Jumanne jioni katika barua iliyotumwa kwa vyuo vikuu kutoka kwa wizara ya elimu ya juu, na kulaaniwa na serikali za kigeni na Umoja wa Mataifa.

Tangu kutolewa tangazo hilo, wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu kote nchini wamezuiwa kuingia vyuoni na walinzi wa Taliban.

Kuzuiliwa kwa wanafunzi hao wa kike huenda kutapelekea shida zaidi kwa juhudi za utawala wa Taliban kutaka kutambuliwa kimataifa na kuwaondolea vikwazo ambavyo vinatatiza sana uchumi.

XS
SM
MD
LG