Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 15:22

Wanawake wa Malawi wasaidiwa kujikwamua kiuchumi


Wanawake wakifanya kazi za kilimo nchini Malawi.
Shirika moja lisilo la kiserikali nchini Malawi la kuwawezesha kina mama linavyojitahidi kuwasaidia wanawake maskini, wajane na wanaonyanyswa ili kuwakwamua kiuchumi kupitia mipango maalum ya akiba na mikopo.

maafisa wa shirika hilo linaloitwa Center for Alternatives for Victimized Women and Children wanasema kwa mujibu wa juhudi mpya, inayojulikana kama benki ya kijiji, wanawake wanashawishiwa kuunda makundi kati ya watu 15 mpaka 25 ili kuchangia kiwango maalum cha fedha kinachokubaliwa kila wiki ili kununua hisa.

Hlazulani Malumbo ziba ni mratibu wa shirika hilo katika wilaya ya kusini ya Chiradzulu, moja ya maeneo ambako miradi inatekelezwa.
Wanawake wa Malawi wawezeshwa - 5:17
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:15 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Ziba anasema makato ya riba baadae yanaongezwa katika kiwango cha fedha ambacho mwanachama binafsi anapewa wakati wa kugawana fedha za hisa, ambazo zinakuwa zimewekwa katika kipindi cha mwaka mazima.

Kwa mujibu wa Ziba, zaidi ya wanawake elfu tano kutoka vijiji 81 wamenufaika na program hii, ambayo imeanza mwaka 2010.

Eunice Victory ni mratibu wa mradi wa akiba na mikopo katika maeneo yanayozunguka kijiji cha Chingoli.

Victory mjane mwenye watoto wawili ameiambia sauti ya amerika kuwa amejiunga na program hii mwaka 2011 kwasababu alikuwa anaishi katika umaskini kufuatia kifo cha mume wake na hakuwa na njia ya kuwalipia ada ya shule watoto wake.
XS
SM
MD
LG