Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 05:56

Wanasheria nchini Uganda waandamana kupinga ukatili wa polisi


Waandanmanaji wakiwa katika karandinga la Polisi.
Waandanmanaji wakiwa katika karandinga la Polisi.

Wanasheria waamua kuandamana Uganda kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wanasheria nchini Uganda wanapinga matumizi ya nguvu ya serikali dhidi ya waandamanaji wanaolalamikia bei kubwa za chakula na mafuta.

Zaidi ya wanasheria100 walikusanyika nje ya mahakama kuu ya Uganda Jumatano ambapo waliwalaani maafisa wa usalama na kuanza kile walichokiita mgomo wa siku tatu.

Polisi nchini Uganda wametumia gesi ya machozi, risasi za mpira na risasi za moto ili kuvunja mandamano kadhaa katika mji mkuu Kampala katika mwezi mmoja uliopita. Umoja

Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, ambaye anaongoza maandamano hayo amekamatwa mara nne. Wiki iliyopita, polisi walivunja dirisha la gari lake na walimwagia gesi ya machozi kabla ya kumtia ndani.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema serikali yake haitavumilia maandamano na ametetea hatua za polisi. Analaumu kuwa hali kupanda kwa gharama za maisha nchini Uganda kunatokana na ukame na kupanda kwa bei za mafuta duniani.

Wanasheria wanataka uchunguzi ufanywe kuhusiana na jaji Justine Atukwasa, ambaye wanasema hakuwa muadilifu katika kesi ya Besigye.

Besigye anaongoza upinzani nchini Uganda kwa zaidi ya muongo mmoja. Ameshindwa mara tatu katika uchaguzi wa urais dhidi ya bwana Museveni, ambaye ameiongoza Uganda tangu mwaka 1986.

XS
SM
MD
LG