Wananchi wa Maldives wamepiga kura leo Jumamosi katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali wa rais wa visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi unaoonekana kama vita vya ushawishi kati ya India na China.
Rais Ibrahim Solih anayewania muhula wa pili wa miaka mitano katika visiwa hivi kivutio cha watalii katika Bahari ya Hindi ametetea sera ya India-kwanza wakati alipokuwa madarakani. Anaonekana kuwa mbele kidogo kwenye kura za maoni.
Muungano unaomuunga mkono mpinzani wake mkuu, Mohamed Muizzu, una rekodi ya kuwa karibu na China na umeanzisha kampeni ya iitwayo India out na kuahidi kuondoa uwepo mdogo wa jeshi la India la ndege kadhaa za uchunguzi na baadhi ya wafanyakazi 75.
Muizzu aliingia kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya Rais wa zamani Abdulla Yameen kupigwa marufuku kushiriki uchaguzi na Mahakama ya Juu mwezi Agosti baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi na biashara haramu ya mzunguko wa fedha.
Forum